Friday, September 7, 2012

PENTAGON ATANGAZA KUWAACHA WAKE ZAKE!!!!

                                                      Pentagon
                                              wake zake
MUIMBAJI wa Bendi ya Extra Bongo, Ramadhan Mhoza ‘Pentagon’ amefunguka kuwa amechoshwa na wake zake hivyo hana muda mrefu atawatimua wote ili aishi peke yake.
Akichonga na gazeti hili juzikati, Pentagon alisema awali alidhani kuwaoa wanawake hao ambao ni Baby Mai na Rahma wangemuongezea furaha katika maisha yake lakini matokeo yake wanamtia kichaa.
Alisema kitu kikubwa kinachomfanya afikirie uamuzi huo ni wivu uliopitiliza hadi kuwa kero kwake na kumfanya ashindwe kufanya mambo yake kiufasaha.
 “Nimeamini kweli wanawake ni pasua kichwa kwani wanaoneana wivu wa kijinga wanabaki kuniumiza kichwa tu mimi, kuanzia mwezi ujao naanza kuishi singo, nitaondoka nyumbani nikatafute sehemu niishi peke yangu nitulie kimya,” alisema Pentagon.
chanzo:http://www.globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment